| Mwenyekiti wa Chama Cha Wanasheria Wanawake Maria Kashonda (katikati) akisoma taarifa kwa waandishi wa habari leo Idara ya Habari Maelezo kuhusu jukwaa la kijinsia la katiba, Gender Forum Constitution Review (GFCR) jukwaa ambalo limeundwa na TAWLA kwa kushirikiana naAsasi zisizo za Kiserikali (NGO's). Akielezea malengo ya kuundwa kwa jukwaa hilo alisema kuwa lengo ni kutoa msukumo na msisitizo kwa Serikali kushirikisha makundi ya kijinsia hususani wanawake katika mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya. Wengine ni Magdalena Kamugisha (Kushoto) ambaye ni mweneykiti wa (GFCR) na kulia ni Bi Victoria Mandari. |
No comments:
Post a Comment