Watanzania: Seattle, WA na Portland, OR
Kwa niaba ya Mwenyekiti TANZASEATTLE nawakumbusha kuwa sherehe zetu za Muungano ni Jumamosi hii tar. 30/4/2011 katika ukumbi wa Eritrean Association Hall (1528 Valentine Place South, Seattle, WA, 98144). Sherehe zitaanza saa kumi jioni.
Kiingilio ni dola 15 (utapata chakula, utaburudika kwa fashion show, utapata burudani ya ngoma, utacheza muziki mpaka majogoo). Vinywaji vitauzwa ukumbini (maji na soda ni dola moja moja, bia dola 3). Tutapokea cash au check tu.
Niwakumbushe tu kuwa Fashion show itaongozwa na dada ASIA IDOROUS- KHAMSIN kutoka Taxes, Ngoma na Mr. Kedmon Mapana (Jiandae kucheza ngoma, usisahau khanga za kujifunga) , Muziki na DJ Dully).
Tafadhali usikose, alika jamaa na marafiki (wageni wote watalipa kiingilio kama kawaida) ================= NJOO TUSELEBUKE |
No comments:
Post a Comment