Thursday, April 28, 2011

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Tanzania Gender Networking Programme (TGNP)

P.O. Box 8921, Dar es Salaam, TANZANIA; Gender Resource Centre, Mabibo Road, Tel. 255 022 2443205/2443286/2443450;
Mobile 255 0754 784050, 0715 784050; 0784 784050 Fax 255 022 2443244; Email info@tgnp.org ; web www.tgnp.org

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Uchambuzi wa seria ya KILIMO KWANZA,Ajira, Biashara na Maisha
Endelevu

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), umezindua muhtasari ya uchambuzi wa sera ya
KILIMO KWANZA: Maana na umuhimu wake kwa jamii iliyoko pembezoni,
Wanawake, Wanaume wa Tanzania na Ajira, Maisha endelevu na Biashara

Muhutasari huu umelenga kutoa uch
ambuzi yakinifu wa sera za serikali na mgawanyo wa bajeti katika sekta hizi mbili
muhimu. Ajira na Maisha Endelevu na Kilimo, kwani zina mahusiano ya karibu
na maendeleo ya wanawake walioko pembezonina wanaume; na ni kitovu cha
kampeni yetu ya: “Haki ya Uchumi: Rasilimali ziwanufaishe wanawake walioko
pembezoni.

Kila muhtasari wa uchambuzi wa sera tulioufanyia kazi uliuliza maswali kadhaa kuwa
ni kwa kiasi gani sera hizi zinaweka vipaumbele mahitaji muhimu ya wanawake hasa
wa kipato cha chini wa vijijini na mijini sio tu kinadharia bali kwa mikakati imara ya
mgawanyo sawa wa rasilimali?

Idadi kubwa ya wanawake wa Kitanzania wanategemea kilimo cha mikono kwa
maisha endelevu, kama chanzo cha kujipatia kipato, pia kama chanzo cha chakula
cha kila siku kwa familia na jamii. Pia idadi kubwa ya wanawake na wanaume bado
imeendelea kutegemea sekta ya kipato isiyo rasmi kama chanzo cha kujipatia kipato
kwa ajili ya mahitaji ya kila siku kwa wote wanaoishi vijijini na mijini

TGNP katika uchambuzi huu wa sera hizi mbili, tumeona kuwa sera na bajeti
zinaweka kipaumbele madai na mahitaji ya makampuni makubwa ya nje na ndani
kama msingi wa kuendesha na kukuza biashara ya nje. Kutokana na kipaumbele
hiki umuhimu wa kusimamia ukuaji wa
uchumi wa Taifa kwa kujitegemea
umesahaulika pamoja na mkakati wa maendeleo ya wananchi wenyewe. .

Lengo kuu la sera
ya KILIMO KWANZA
ni kuweka nguvu kwa
wazalishajiwakubwa kwa kuwapa kupata vipaumbele kutoka serikalini hasa katika
maeneo ya mikopo, misamaha ya kodi, ruzuku na nyinginezo. Pia wamekuwa
wakitumia njia hiyo kudai soko huria katika ardhi, umiliki wa ardhi, kwa kigezo kuwa
watawafikia wananchi wa hali ya kawaida walioko vijijini.

Changamoto kubwa katika sera hii ya sasa ya KILIMO ni jinsi inavyoonekana
kukubali na kuukabiribisha mfumo mpya wa matumizi ya mbegu zilizorekebishwa
– “genetically modified seeds” (GM), maarufu kama “mbegu za miujiza” (Miracle
Seeds), unaolenga kuzalisha mbegu za mazao katika maabara, kilimo cha mazao ya
nishati (Biofuel), matumizi makubwa ya mbolea za viwandani na madawa ya kilimo.

Uchambuzi uliofanywa kuhusu mfumo huu hapa Afrika na Asia umeweka wazi
athari na changamoto za tekonolojia hii ya uzalishaji mbegu inayomlazimisha
mkulima mdogo kuwa na majukumu makubwa kinyume na uwezo wake. Mfumo
unaelekeza nguvu zake katika kilimo kikubwa wakati walengwa ni masikini. Hatua
hii inapelekea mashirika makubwa yanayojihusisha na kilimo na biashara kunufaika
kupitia ukodishaji wa mashamba, uuzaji wa pembejeo, madawa na mbolea na
kuwaacha wakulima masikini mikono mitupu.

Wakati mwingine hawa ndio wamekuwa wananunuzi wa kubwa wa mazao
yanayozalishwa kwa kulangua, mabenki makubwa pia yameonesha kunufaika zaidi
kuliko mwananchi masikini kutokana na kudai riba kubwa katika mikopo ya kilimo
hasa hiki cha uzalishaji wa mbegu.

Mfumo huu wa mbegu za GM umekuwa kikwazo kwa wakulima wadogo kwa
sababu hawawezi kuhifadhi mazao yao ili kuandaa mbegu kwa ajili ya msimu
unaofuata, kwa hiyo unawalazimisha wakulima wadogo kuendelea na mtindo wa
kununua mbegu madukani kila mwaka badala ya kuzalisha za kwao kwa njia za asili.
Athari nyingine ni matumizi ya zana kubwa katika kilimo kinachotumia mitambo na
mafuta, hivyo kusababisha makampuni makubwa ya mafuta kujiingiza humo, kama
wanufaika wakubwa na hivyo kujenga nguvu kubwa ya ushawishi ya kuendeleza aina
hii ya kilimo.

Ili kutimiza hili, sehemu ya ardhi ya kilimo cha chakula lazima itumike, na hivyo
mkulima kulazimika kugawa muda wake kati ya kilimo cha mazao ya biashara ambayo
serikali inayataka (na kwa yeye kupata fedha kulipia kodi), na kilimo cha chakula kwa
ajili ya familia yake.

Kwaupande mwingine kukimbilia teknolojia hii, serikali inajivua wajibu wa
kumwendeleza mkulima mdogo na kufungua milango kwa masetla; hivyo kumfanya
abaki kibarua kwenye ardhi yake aliyoirithi.

Mfumo wa GM umekuwa ukishinikizwa Tanzania na nchi jirani na Jumuiko la
Mapinduzi ya Kijani Kibichi Afrika, (AGRA), Ukuzaji wa Kilimo katika mwambao
wa Kusini na mashirika makubwa ya kilimo cha biashara. Banki ya StanBanki na
kampuni za Monsanto, SAB Miller, Diageo, Syngenta na General Mills, wamewekeza
kwa kiasi kikubwa kwenye kilimo ambacho hakitoi usalama wa chakula wala ajira kwa
Watanzania, bali ni kunufaika katika kuuza chakula nje na mzao ya nishati mbadala na
kuongeza bei ya chakula katika soko la ndani.

Uchambuzi wetu wa Sera ya Ajira, Maisha na endelevu na Biashara umeongozwa
na swali je,ni mikakati gani imewekwa ya kuongeza Ajira na maisha endelevu kwa
Watanzania wote wanawake na wanaume? Mtazamo wa serikali na mwelekeo wake
umeonekana kuwa ni kuangalia vikundi vidogo vya uzalishaji ambavyo hata hivyo
wanaonufaika nao ni wanawake na wanaume wajasirimali wenye uwezo walioko mijini
wakati walio wengi vijijini wakiwa wameachwa.

Kwa sasa idadi kubwa ya wanawake na wanaume wa vijijini na mijini
wamenyang’anywa kila fursa ya uzalishaji kwa ajili ya maisha endelevu, kama vile
ardhi, maji, misitu, nk. Athari hizi ni matokeo ya unyang’anyaji wa ardhi za wananchi,
mikakati ya mipango miji, kukimbizwa na kufukuzwa kwa wamachinga, vibanda
vidogo, bomoa bomoa na kuingiza ardhi katika biashara huria. Wakati huo huo
mfumo wa uchumi kuuza mazao nje ya nchi bila mkakati mathubuti ya kuendeleza
soko la ndani unaendelea kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha tabaka kati ya
masikini na tajiri kwa wote wanaoishi vijijini na mijini.

Katika mkanganyiko huu wanawake wanakumbana na changamoto zaidi
zinazotokana na mfumo dume ulioko serikalini na katika taasisi za kijamii kwa kupata
nafasi chache za ajira, mikopo, ardhi, na elimu kuliko wanaume.

Kwa mfano katika kiwango cha asilimia 14 ya masaa yote ya ya siku wanawake
huwa wanafanya kazi isiyo na malipo, wakati wanaume ni asilimia 5 tu ya muda wao
hutumika kufanya kazi za nyumbani zisizo na malipo. Utafiti wa kitaifa wa soko
la ajirawa mwaka 2006, uliainisha kwamba asilimia 66 ya wanaofanya kazi kama
wasaidizi kwenye familia bila malipo ni wanawake. Wakati huo huo, taratibu wa
kumiliki na kurithi ardhi ya familia unaendelezwa kwa kufuata mfumo dume wa mila
na desturi ambazo zinawanyima haki wanawake.

Wanaharakati wa kifeministi wanaamini kuwa Watanzania wote wanaume na
wanawake wana haki sawa ya kupata ajira na maisha endelevu. Kufikia ajira kwa wote
kunategemea mabadiliko ya kisasa katika mikakati ya maendeleo sera za nchi.

Imetolewa na:

Usu Mallya

…………………

Mkurugenzi Mtendaji

No comments:

Post a Comment