Monday, April 25, 2011

Tamasha La Pasaka Jana Diomond Jubilee... Wengi Waliishia Nje

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Bon Mwaitege na vijana wake wacheza shoo hawakupata upenyo wa kuingia ukumbini. Ukumbi ulijaa mapema na askari waliokuwa mlangoni waliwazuia watu kuingia ndani licha ya kuwa tayari walikuwa na tiketi.
Msururu wa wapenzi wa nyimbo za Injili wakiwa wanapigania kuingia ndani ya ukumbi wa Diomond Jubilee jana wakati wa Tamasha la Pasaka. Kutokana na idadi kubwa ya mashabiki na ukumbini, mashabiki wengi walishindwa kuingia hali iliyopelekea  kuzuka patashiki  baina ya mashabiki na askari waliokuwa wakilinda usalama.Mashabiki wakidai kurudishiwa  pesa za viingilio. Katika tamasha hilo lililoandaliwa na Misama Promotion mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Kikwete.

No comments:

Post a Comment