Saturday, April 30, 2011

Watatu Raia Mwema Kuwania Tuzo Ya Wanahabari


Pichani ni Johnsson Mbwambo, Mwandishi mwandamizi na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Raia Mwema.

Raymond Kaminyoge
WAANDISHI habari tisa wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd ni miongoni mwa walioteuliwa kuwania tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT).

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), John Mireny alitangaza majina hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari na kufafanua kuwa tuzo hizo zitatolewa Jumanne ijayo ambayo ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.


Mireny alitaja majina ya waandishi wa Mwananchi Communications Ltd kuwa ni Bernard James (utawala bora), Rashid Kagusa (katoni) na Samuel Mwamkinga (katoni).Walioteuliwa kushindana katika kundi la malaria ni Leon Bahati na Lucas Liganga wakati katika kundi la wenye ulemavu mwandishi aliyeteuliwa ni Tumaini Msowoya.

Mireny aliwataja waandishi wengine wa Mwananchi kuwa ni Frolence Majani (habari za jinsia), Lucas Lugakingira (habari za afya) na Sheila Sezzy (habari za mazingira).

Aliwataja washindi walioteuliwa kugombea nafasi za jumla kutoka katika vyombo vingine vya habari kuwa ni Angelo Mwoleka (Star TV), Masoud Masoud (TBC 1), Orton Kiishweko (Daily News), Grace Kiondo (Zenj FM), Dorcas Raymos (Channel 10) na Martin Kuhanga (Radio Tumaini).

Kwa mujibu wa Mireny waandishi wa vyombo vingine vya habari na majina ya vyombo wanakotoka walioteuliwa kuwania nafasi katika makundi mbalimbali ni Nathan Mpangala (ITV), Robert Okanda (Daily News) na Bashir Nkoromo (Uhuru/Mzalendo).

Wengine ni Mbaraka Islam (Raia Mwema), Orton Kiishweko (Daily News), Mbazigwa Hassan (TBC Taifa), Joseph Burra (TBS Taifa) na Sima Bingileki (Iringa Municipal TV).
Wengine waliotajwa ni Margreth Tengule (Star TV), Sam Mahela (ITV), Festo Sikagonamo (ITV), Deogratius Mushi (Daily News) na Dorice Malima (TBC1).

Kaimu katibu mkuu huyo aliwataja waandishi wengine kuwa ni Masoud Masoud (TBC1), Malima Bundala (TBC Taifa), Victoria Patrick (TBC1) na Sabina Wandiba (Changamoto).

Wengine ni Edwin Ndeketela (TBC FM), Tuma Dandi (Radio Mlimani), Samwel Chamlomo (TBC1), Stella Setumbi (TBC Taifa), Dorcas Raymos (Channel 10) Sabina Hading’oka (Uhuru) na Grace Kiondo (Zenj FM).
Wengine ni Amina Mollel (TBC1), Elesia Isabula (TBC Taifa), Rose Mdami (Tumaini TV), Jackson Jackson (Mlimani Radio), Martin Kuhanga (Radio Tumaini) na Dotto Mnyadi (TBC1).

Mireny aliwataja wengine kuwa ni Dorice Kaunda (TBC Taifa), Lina Denis (Channel 10), Aloysia Maneno (TBC Taifa) Elisia Isabula (TBC Taifa), Godfrey Nago (TBC 1), Angela Akilimali (Uhuru FM), Felix Mwakyembe (Raia Mwema) na Musa Twangilo (TBC Taifa).

Waandishi wengine ni Saleh Masoud (Mlimani TV), Emmanuel Chacha (Raia Mwema), Ezekiel Kamanga (Baraka FM Mbeya), Bilal Abdul Azizi ( (The Guardian), Adeladius Makwega (TBC Taifa) Agnes Tuniga (TBC 1) na Happy Mollel (Nipashe)

Aidha, wengine kwa mujibu wa Mireny ni Pius Ntiga (Radio Uhuru), Maliganya Charahani (Star TV), Gervas Hubile (TBC Taifa), Angelo Mwoleka Star TV na Victoria Patrick (TBC Taifa).

Mireny alisema washindi wa tuzo hiyo watatokana na majina yalioteuliwa na watapewa tuzo kwenye sherehe za uhuru wa vyombo vya habari itakayofanyika Jumanne ijayo.
Alisema kazi zilizoshindanishwa ni 437 kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari.

Alisema Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta amekubali kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo zitakazofanyika katika ukumbi wa Mlimani City.

“ Wanahabari wote nchini mnaalikwa kuhudhuria sherehe hizo bila kukosa,” alisema Kaimu Katibu Mkuu wa MCT. CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment