Monday, April 25, 2011

Askofu Valentino Mokiwa: Bunge Sasa Ni Kama Shule Ya Msingi

ASKOFU Mkuu wa Anglikana Tanzania, Valentino Mokiwa
--  
ASKOFU Mkuu wa Anglikana Tanzania, Valentino Mokiwa amewashukia wabunge kwa tabia yao ya kuzomeana wakati vikao vya Bunge hilo vikiendelea, akisema hali hiyo inawashushia heshima ya uwakilishi wa wananchi waliyonayo. 

Pia Askofu huyo ameweka bayana kuwa anachukizwa na kitendo cha mgawo wa umeme na kuitaka Serikali kuacha kuegemea zaidi katika uzalishaji umeme wa maji kwa kuwa ukosefu wa umeme pamoja na kuchangia kurudisha maendeleo, pia ni chanzo cha ukosefu wa amani nchini. 

Akizungumza katika Ibada ya Misa ya Pasaka katika Kanisa la Mtakatifu Albano Dayosisi ya Dar es Salaam, amesema kwa sasa vyombo vingi vya Dola vimekuwa vikitenda mambo kinyume cha taratibu zinazotakiwa, jambo ambalo pamoja na kuvishushia hadhi, pia linachangia kuleta machafuko ya amani. 

“Sote tumeshuhudia juzi namna Bunge lilivyopoteza thamani na heshima yake na kuwa kama shule ya msingi, wabunge wanazomeana kama watoto wadogo, natamani Mwalimu Nyerere angekuwa hai….soma zaidi http://www.kwanzajamii.com

No comments:

Post a Comment